Mwanamuziki, Rico Single kutoka visiwani Zanzibar amesema kuwa kuimba wimbo wa harakati kama alivyofanya Nay wa Mitego ni vigumu kwa Zanzibar kutokana na mitazamo tofauti ya siasa.
Rico Single amesema hayo baada ya hivi karibuni Nay wa Mitego kukamatwa na jeshi la Polisi baada ya kuachia wimbo wake ‘Wapo’ unaodaiwa kuikashifu Serikali iliyopo madarakani.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa sema siasa visiwani Zanzibar ina nafasi kubwa sana na ikitokea msanii kuimba wimbo kama huo, huenda akakutana na matatizo makubwa kutoka kwa mtu mmoja mmoja hata kama si mlengwa aliyeimbiwa wimbo huo.
“Huku bana watu wanapenda siasa kuliko fedha, ukiimba harakati kama za wimbo wa Nay utajikuta katika matatizo, maana mtu tu mwenye mapenzi na unayemuimba anaweza kukudhuru kabla hata mlengwa mwenyewe hajakufikia, ndiyo maana harakati huku zimepungua kwa wasanii,’’.
Rico Single amesema kuwa baadhi ya wasanii Visiwani humo walishawahi kuimba nyimbo zenye ujumbe wa harakati kwa kuikumbusha serikali mambo maovu yanayofanywa na watu visiwani humo, lakini mapokeo yake yakawa tofauti.