Mtoto wa Rais wa Marekani, Donald Trump aitwae Ivanka Trump amechaguliwa kushika nafasi ya msaidizi wa baba yake katika Ikulu ya Marekani ‘White House’.

Ivanka amekubali shinikizo baada ya wataalamu kuhusu maadili kukosoa mpango wake wa awali wa kutaka kuhudumu katika wadhifa usio rasmi.

Binti huyo wa Trump mwenye umri wa miaka 35 amesema kuwa amesikia maswali ambayo baadhi ya watu wamekuwa wakimuuliza kuhusu hatua yake ya kumshauri rais katika nafasi kama mtu binafsi”.

Kupitia taarifa, White House imesema ina furaha kwamba “Ivanka Trump amechukua hatua hii isiyotarajiwa katika nafasi yake kama binti wa rais”.

Bi Trump alisema kupitia taarifa yake kwamba amekuwa akifanya kazi “kwa nia jema na kundi la washauri wa rais White House pamoja na mshauri wake binafsi kujadili kuhusu jukumu lake”.

Wataalamu kuhusu maadili walilalamika ilipobainika wiki iliyopita kwamba Bi Trump angepewa afisi White House pamoja na kibali cha usalama cha kuingia na kuondoka ikulu hiyo, bila yeye kujiunga rasmi na wahudumu wa rais.

Wakosoaji walisema kazi ya Bi Trump inafaa kufanywa rasmi ndipo aweze kudhibitiwa na sheria kuhusu uwazi wa maafisa wa serikali pamoja na maadili.

Wakili wa Bi Trump, Jamie Gorelick, amesema mteja wake atawasilisha nyaraka zifaazo za kufichua utajiri wake kwa mujibu wa sheria kuhusu maadili ya watumishi wa umma Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *