Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli jana amefungu kikao cha pamoja cha Mawaziri wa Serikali za Tanzania na Uganda pamoja na wadau kuzungumzia mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Mkutano huo, uliofanyika Ikulu, Dar es salaam ulihudhuriwa na Mawaziri wa Nishati na Madini pamoja na Mawaziri wa Ardhi wa nchi hizo mbili, Wanasheria wa Serikali  na kampuni washirika wa mradi huo Lake Albert (CNOOC, TOTAL na TULLOW).

Pamoja na mambo mengine, Mawaziri, Maafisa na Wataalam wa pande zote husika walikaa na kukubaliana kwamba rasimu ya  makubaliano rasmi ya kuanza kwa mradi yawe yamekamilika na kuwa tayari katika kipindi cha wiki mbili.

Marais wa Tanzania na Uganda wanatarajia kuweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa kihistoria wa mradi huo wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *