Staa wa Hip-Hop nchini, Joseph Haule  “Profesa J” ameusifia muziki wa singeli umbao unafanya vizuri sana katika jiji la Dar es Salaam kwasasa tofauti na mikoa mingine hapa nchini.

Profesa Jay ambaye ni mbunge wa Mikumi mkoani Morogoro amesema ni bora kuchanganya Hip-Hop na muziki huo kuliko kuiga wasanii wa nje.

Staa huyo amesema kwamba amefanya Hip-Hop singeli kwa ajili ya kuupeleka muziki mbali na pia kuipeleka Hip-Hop tofauti na hapo awali ni bora zaidi kuliko kuiga wanavyoimba wasanii wa Marekani.

Profesa Jay ameongeza kwa kusema watanzania tumekuwa na muziki aueleweki hata Hip-Hop wanayoifanya inaweza kumtambulisha huyu ni matanzani ni lugha ya kiswahili tu na siyo radha wala mdundo wa nyimbo.

Ivi Karibuni Profesa Jay alishoot video ya wimbo wake aliyomshirikisha mwanamuziki wa singeli, Shoro Mwamba na kuimba mahadhi ya Singeli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *