Baada ya beki wa timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland na klabu ya Everton, Seamus Coleman kuvunjika mguu, Shirikisho la Soka Dunia (FIFA) limesema litamlipa kwa kipindi chote atakacho uguza jelaha lake la mguu.

Beki huyo alivunjika mguu wa kulia katika mechi dhidi ya Wales baada ya kuchezewa rafu na beki Neil Taylor wiki iliyopita.

Coleman alifanyiwa upasuaji na sasa anataraji kukaa nje ya uwanja kwa muda wa takribani miezi 6 akijiuguza jeraha hilo.

FIFA kupitia (Fifa Club Protection Programme) wamethibitisha watakuwa wanamlipa mchezaji huyo kwa kipindi hicho chote atakachokuwa nje

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *