Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambaye alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi kuhusiana na wimbo wake ameachiliwa huru.

Nay Wa Mitego ameachiliwa huru saa chache baada ya Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe kuagiza aachiliwe huru.

Baada ya kuachiwa Nay wa Mitego amesema “Saa hizi sina kubwa la kuongea. Wimbo umeruhusiwa. Nashukuru. Nafurahi kusikia taarifa ya serikali kwamba wameruhuru wa Wapo upigwe. Upigwe kwa nguvu,”.

Kuhusu kuuboresha wimbo huo, amesema: “”Hili nitalifanyia kazi. Siwezi kusema saa hizi ni vitu gani kwa sababu ndio nimetoka huko. Lakini nitalifanyia kazi kwa sababu tayari ni wimbo wa kila mtu, wimbo wa Watanzania, wimbo wa watu wote.”

Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *