Kamaati ilyoundwa na waziri mkuu, Kassim Majaliwa kuchunguza kifo cha Faru John imetoa taarifa kuwa mnyama huyo alikufa hifadhi ya Sasakwa Gruneti kwa kukosa matibabu wakati alipoumwa.
Akiwakilisha ripoti hiyo kwa waziri mkuu, mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samwel Mnyele amesema kuwa Faru John alikosa matunzo na uangalizi wa Karibu.
Mnyele ambaye ni mkemia mkuu wa Serikali amesema kuwa hakukuwa na kibali rasmi cha kumuamisha Faru John kutoka Ngorongoro kwenda Gruneti.
Kamati hiyo imesema kuwa hatua za kiutawala zichukuliwe dhidi ya ofisi ya mkurugenzi wa Wanyamapori na Mhafadhi wa Ngorongoro kutokana na na mapungufu yaliyojitokeza.
Kwa upande wake waziri mkuu, Kassim Majaliwa ameishukuru kamati kwa kazi hiyo na kusema kuwa Serikali itaifanyia kazi mapendekezo ili kulinda Maliasili.