Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) limesema kuwa shirika la Umeme nchini Tanesco linawadai deni la shilingi bilioni 3 kutokana na matumizi ya umeme.
Hayo yamesemwa na mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama, Evance Mabeyo mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi amesema kuwa deni hilo limetokana na shughuli za jeshi kwenye ulinzi wa jeshi pamoja na ufinyu wa bajeti.
Mabeyo amesema kuwa kesho wanatarajiwa kupunguza deni hilo kwa kulipa shilingi bilioni moja ili wasikatiwe umeme.
Mwisho mkuu wa Majeshi huyo amesema kuwa juhudi zinazofanywa na jeshi hilo zinatakiwa kuoneshwa na taasisi nyingine ili kuweza kuiongozea Tanesco uwezo wa kutoa huduma.