Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe ameshangazwa na idara ya elimu msingi ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kushindwa kumchukulia hatua Mwalimu aliyekutwa amelewa wakati wa kazi.

Mwalimu huyo, Fikiri Swai wa Shule ya Msingi Kwankonje, anatuhumiwa kufika kazini akiwa amelewa pombe.

Tukio hilo lilitokea juzi shuleni hapo wakati Gondwe alipofika katika mpango wa kusambaza mbegu za mihogo na katika shughuli hiyo, alifika mwalimu huyo na kuanza kusalimia akiwa amelewa chakari.

Kutokana na hali hiyo, Gondwe alitaka kufahamu kama ni mwalimu wa shule hiyo na ndipo alipojibiwa kuwa ndiyo na kuelezwa kuwa
hiyo ni tabia yake ya muda mrefu. Pia ilielezwa kuwa ameshachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo kusimamishwa kazi.

Baada ya majibu hayo, Gondwe alisema mtumishi wa umma kufika kazini akiwa amelewa au kufanya hivyo muda wa kazi na kwamba kitendo cha mwalimu huyo ni kosa na ameonyesha dharau mbele ya viongozi wa ngazi ya juu ndani ya wilay.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *