Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt John Pombe Magufuli ametoa onyo kwa vyombo vya habari nchini kwa madai ya kuandika habari zisizo za kizalendo.

Rais Magufuli amesema hayo baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali katika ukumbi wa mikutano, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kiongozi huyo amemtaka waziri mpya wa Habari Dkt Harrison Mwakyembe kuvichukulia hatua za kisheria vyombo vya habari vitakavyoonekana kutumia visivyo khaki ya uhuru wa kupasha habari.

“Kila kitu chenye nia ya uchochezi fulani fulani, wao ndio stori. Sasa Mwakyembe kafanye kazi. Nataka ukafanye kazi. Kama wapo waliokuwepo waliokuwa wanashindwa kuchukua hatua wewe kachukue,” ametoa maelekezo rais Magufuli.

“Kwani ni mwanasheria mzuri, msomi, umesomea mambo ya habari, kafanye kazi. Serikali ipo. Hatuwezi tukaiacha serikali ikaangamia kwa sababu ya watu wachache.” Ameongeza rais Mgufuli.

Rais Magufuli ameonyesha kuchukizwa na habari zilizopamba kurasa za juu katika magazeti ya leo ambapo magazeti mengi yameweka picha ya aliyekuwa waziri wa habari Nape Nnauye akionyeshwa bastola na askari kanzu jaribio lake la kufanya mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia sakata la kutenguliwa kwa uteuzi wake.

“Hata kasomeni tu magazeti ya leo. Picha yote heading ni picha ya mtu ambaye alifanya kosa moja, kana kwamba kitendo hicho kilifanywa na serikali. Ukurasa wa kwanza, ukurasa wa pili, huyu anatoa anafanya hivi….nawaambia wamiliki wa vyombo vya habari, tahadharini. Kama mnafikiri mna uhuru wa namna hiyo, haujafikia huko.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *