Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limempongeza Dkt Harrison Mwakwembe baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, akichukua nafasi ya Nape Nnauye.
Dkt. Mwakiyembe aliyekuwa waziri wa Katiba na Sheria amebadilisha nafasi hiyo huku akihamishwa kwenye wizara iliyokuwa inaongozwa na Nape Nnauye.
Kupitia akaunti ya twitter ya Rais wa Shirikisho hilo, Jamal Malinzi amesema TFF inampongeza Mwakiyembe kwa kuteuliwa kuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.