Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linatarajia kutoa tuzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari nchini waliofanya vizuri kitaifa katika masomo ya Sanaa za Muziki, Ufundi na Maonyesho kwenye matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana.
BASATA watatoa vyeti na zawadi za fedha taslimu kwa wanafunzi hao pia Baraza hilo litatambua mchango wa walimu wa masomo husika na shule zilizofanya vizuri katika masomo ya Sanaa.
Sherehe ya kukabidhi tunzo hizo zitafanyika siku ya Jumatatu ijayo tarehe katika Ukumbi wa BASATA ulioko Ilala jijini Dar es Salaam.
Baraza hilo limeamua kurejesha programu hii ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari kila mwaka ambao wanashika nafasi za juu kitaifa katika masomo ya sanaa husasan Sanaa za Ufundi, Maonyesho na Muziki.
BASATA limekuwa na mwendelezo wa programu mbalimbali za Sanaa kwa watoto zilizoanza tangu miaka ya 1980 ambazo zimepata kuibua na kukuza vipaji vya wasanii.