Mbunge wa Nzega mjini, Hussein Bashe amempongeza Waziri wa Habari, Nape Nnauye kutokana na kamati yake kukamilisha ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Clouds Media.
Kupitia akaunti yake ya Twitter Bashe ameandika ujumbe wa kumpongeza Nape kwa kumwambia kuwa amelinda heshima ya tasnia ya habari.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amekabidhiwa ripoti na Kamati aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza tukio la tuhuma za uvamizi uliofanywa na mkuu wa mkoa huyo.
Waziri Nape baada ya kupokea ripoti hiyo aliongea na Waandishi wa Habari kueleza kuwa hatua inayofuata ni yeye kuiwasilisha ripoti hiyo katika ngazi kuu ya uongozi akiwemo Rais Magufuli ili hatua stahiki iweze kuchukuliwa.