Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema suala la uvamizi wa kituo cha Clouds Tv wahusika wanatakiwa kuripoti tukio hilo Polisi haraka.
Kamanda Sirro amesema atafuatilia kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda kama tayari limeripotiwa kwa hatua zaidi.
Hatua hiyo imekuja kufuatia kwa kuenea habari inayomuhusu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media zilizopo maeneo ya Mikochoni B akiwa na askari wenye silaha za moto.
Mkuu wa mkoa huyo alivamia ofisi za Clouds Media kutokana na kutorushwa kwa habari yenye mahudhui kuhusu Grace Athumani anayedaiwa kuzaa na mchungaji wa kanisa la Ufufuo na Uzima mchungaji Josephat Gwajima.
Kulingana na ripoti ya kamati ya watu watano iliyochaguliwa na Waziri wa Habari, Nape Nnauye imethibitisha mkuu wa mkoa alifanya tukio hilo mida ya saa nne na nusu usiku wa Ijumaa tarehe 17 mwaka 2017.