Mwanamuziki chipukizi wa Bongo Fleva, Harmorapa amesema kuwa watu wanaomuongela vibaya ndiyo wanazidi kumpa umaarufu.
Harmorapa amesema hayo baada ya watu kumuongelea vibaya kuhusu jinsi alivyo umbile lake mpaka kupelekea dansa wa Diamond, Moses Iyobo kumfananisha na nyani.
Mwanamuziki amesema kuwa “Watu ambao wanahisi Harmorapa hatodumu kwenye game kwanza wanakosea halafu pia naweza nikasema kwamba wanamkufuru Mungu kwa sababu “.
“Kama mimi binafsi nimejipanga sana vya kutosha. Unajua kwamba maneno yao mimi hayanivinjii chochote ni ile sawa na kumpiga chura teke na kumwongezea mwendo. Wanavyoniongea mimi ndo wananipa power na wananipa maujuzi na wananipa kuweza. Ni wao wananiweza mimi kuweza na kukaza ilmradi niweze kufanya kazi nzuri.”
Harmorapa amesema kuwa hakuwa akimfahamu muimbaji kutoka WCB, Harmonize kabla hajatoka na kuwa maarufu.
Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake ‘Kiboko ya Mabishoo’ aliyomshirikisha mkongwe Juma Nature.