Makamu rais wa zamani wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Jean-Pierre Bemba, anatarajiwa kuhukumiwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC leo baada ya kubainika na hatia ya kutoa hongo kwa mashahidi na kutoa ushahidi wa uongo.
Katika kesi ya kwanza kuwahi kusikilizwa kuhusu ufisadi mahakama hiyo ilimsikiliza Bwana Bemba na washirika wake wanne waliopewa hongo na kuweza kuwafanya mashahidi muhimu wapatao wanne wabadilishe ushahidi wao katika kesi ya uhalifu wa kivita dhidi yake mapema mwaka huu.
Tayari ametumikia miaka kumi na minane ya kifungo chake gerezani kwa uhalifu huo wa kivita.
Bemba, wakili wake, meneja wa kesi yake, mwanasiasa mwingine na shahidi wa upande wa utetezi wote wanakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela , faini ama adhabo zote kwa pamoja.