Mbunge wa Chalinze, Ridhwani Kikwete amesema kuwa taarifa za kuhusishwa na uuzaji wa dawa za kulevya zilitingisha familia yake lakini baba yake alimtia moyo kuhusu suala hilo.
Ridhwani amesema kuwa baba yake ambaye ni Rais mstaafu, Jakaya Kikwete hakushtushwa na habari hizo badala yake akampa nguvu ya kwenda kueleza ukweli kuhusu sakata hilo la madawa ya kulevya.
Amesema kuwa sababu ya Kikwete kutokuwa na hofu labda alitaka kumtia nguvu kwenye suala hilo.
Mbunge huyo aliitwa na mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya kwa ajili ya mahojiano kuhusu kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Baada ya mahojiano hayo Ridhwani ameonekana hana hatia na akachiwa na kuendelea na shighuli zake kama kawaida.
Ridhwani ni miongoni mwa majina yaliyokabidhiwa kwa mkurugenzi wa mamlaka ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya, Rogers Sianga kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.