Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameonesha nakala ya cheti cha matokeo ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne (CSEE) alichodai kuwa ni cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Katika siku za karibuni, Askofu Gwajima kwa nyakati tofauti akiwa kanisani kwake alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa anatumia vyeti vya mtu mwingine aitwaye Paul Christian Malanja wakati jina lake halisi ni Daudi Albert Bashite.

Akizungumza kanisani kwake Ubungo Dar es Salaam jana, kwenye ibada aliyoipa somo lisemalo ‘Nitavunja vunja magari ya chuma’ Gwajima alidai cheti hicho ni nakala halali ambayo ilitolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa Shule ya Sekondari ya Pamba Mwanza ambako Makonda alisoma.

Aliongeza “Hiki ndicho cheti chake halali, watu wanasema Gwajima huogopi kufa, mimi siogopi kufa…. ‘let me say something’, unaweza kuua mwili wangu lakini huwezi kuiua roho yangu, nitaendelea kuwepo.

Amesema anashangazwa na ukimya wa Rais Magufuli dhidi ya Makonda, kwani ni zaidi ya wiki tatu sasa Makonda amekuwa akilalamikiwa kuhusu kutumia vyeti vya mtu mwingine hata hivyo hajamchukulia hatua yoyote kama alivyofanya kwa wengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *