Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media, Ruge Mutahaba amethibitisha ofisi za media hiyo kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Polisi wenye silaha za moto.
Ruge amesema hayo leo kupitia mahojiano na kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Clouds TV na kuelezea yote yaliyotokea siku ya Ijumaa usiku.
Bwana Ruge amesema kuwa alipigiwa simu mida ya saa tano kasoro usiku kutoka kwa HR wa Clouds Media aliyemtaja kwa jina moja la Kitoi akimfahamisha kuwa mkuu wa mkoa ameavamia ofisi hizo zilizopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam akiwa na askari wakiwa na Silaha za moto.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa sababu ya mkuu wa mkoa Makonda kuvamia ofisi hizo ni kutokana kuzuiwa kuruka kipindi cha mkuu wa mkoa huyo kilichokuwa kina muhusu mchungaji Gwajima kuzaa na mwanamke na kumtelekeza.
Ruge amesema kuwa sababu ya kuzuia kipindi hiko kisiruke kwasababu stori hiyo ilikuwa aina balance kutokana na mahujiano hayo kubase sehemu moja tu kwa mwanamke aliyetuhumiwa kuzaa na Gwajima lakini hawakuwa na mahjiaono kutoka kwa Gwajima.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa alipigiwa simu na Gwajima akimuuliza kuwa anasikia kuna habari yake ya kumchafua lakini Ruge alimwambia habari hiyo haiwezi kutoka kutokana na kukosa ukweli.
Ruge amesema kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam alitaka video hiyo ya kumchafua Gwajima irushwe kupitia kipindi cha Shilawadu kinachoruka kila siku ya Ijumaa kupitia Clouds TV.
Pia Ruge amesema kuwa alimpigia simu mkuu wa mkoa huyo na Makonda akaanza kumlaumu kwanini habari yake haikuruka hewani kwenye kipindi cha Shilawadu kinachoongozwa na Qwissah Tompson na Soudy Brown.
Ruge ameongeza kwa kusema kuwa Makonda pia alimpigia simu Mmiliki wa Clouds Media, Joseph Kusaga akimlamu kwanini kipindi chake hakiruki hewani kupitia Shilawadu.
Kuhusu kupigwa kwa watangazaji wa kipindi cha Shilawadu, Ruge amesema kuwa taarifa hizo siyo za kweli na hakuna mtu yoyote aliyepigwa kwenye tukio hilo lililofanywa na mkuu wa mkoa huyo.
Vile vile Ruge amethibitisha kuwa video inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha Makonda akiingia mapokezi ya Clouds ni kweli video hiyo imerekodiwa na CCTV za Clouds lakini amekata kumtaja aliyezivujisha kwenye mitandao ya kijamii.
Kutokana na yote yaloyotokea siku ya Ijumaa Ruge amemtaka mkuu wa mkoa huyo kuomba radhi kwa kilichotokea siku hiyo.