Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekwenda nchini Mauritius kuhudhuria uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi barani Afrika.
Majaliwa amemwakilisha Rais John Magufuli, katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika(The inaugural session of The African Economic Platform).
Waziri Mkuu ameondoka jana kuelekea nchini humo akisindikizwa uwanja wa Ndege na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mauritius inakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika kuanzia Machi 20 hadi 22 katika hoteli ya Turtle Bay, jijini Balaclava.
Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravid Jugnauth atafungua mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na viongozi wakuu wa kisiasa wa Afrika, wafanyabiashara, vyuo vikuu, sekta binafsi na wasomi.