Rais wa Marekani, Donald Trump na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel wametofautiana kuhusu maswala ya uhamiaji, uhusiano wao na Urusi na hata biashara ya kimataifa.
Donald Trump amedai Marekani imekuwa ikipunjwa katika mikataba ya kibiashara iliyoweka saini.
Trump amesema kuwa Amesema sera ambayo amekuwa akiinadi si ya kujitenga bali ni kuelezea kwamba Marekani imekuwa ikionewa na hivyo kutafuta usawa wa haki katika biashara
Kwa upande wake Bi Merkel amehimiza faida za kuendeleza biashara huru ya kimataifa kati ya nchi hizo.
Pia ametoa wito wakimbizi watendewe haki kwa kuwa na uwazi katika kushughulikia maswala yao.
Japo viongozi hao wawili walijitahidi, ni dhahiri bado kuna ukakasi katika uhusiano wao kutokana na jinsi Trump alivyomsema bi Merkel vibaya katika hotuba zake za wakati wa kampeni.