Wajumbe wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo wanafanya uchaguzi wa kumchagua rais pamoja na wajumbe wa ngazi mbalimbali za uongozi wa chama chao.

Uchaguzi huo unafanyika mjini Arusha ambako wanachama wote wa TLS wanakutana kutekeleza ratiba hiyo pamoja na kupanga mipango mbalimbali ya utendaji kazi wa chama hicho.

Kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza chama cha TLS ambacho kilianzishwa mwaka 1954, wajumbe watakaochaguliwa leo watakuwa na dhamana ya kukiongoza chama hicho kwa kipindi cha mwaka mmoja kisha wataachia ngazi hizo ili kupisha uchaguzi mwingine.

Pamoja na kwamba uchaguzi huo utagusa nafasi nyingi za uongozi ambazo zinatakiwa kujazwa, nafasi ya rais wa chama hicho ndiyo inaangaliwa na wengi siku ya leo. Kwamba kati ya wagombea watano waliojitokeza kuwania kiti hicho ni nani atakayeibuka mshindi.

Nafasi hiyo inawaniwa na Victoria Mandari, Tundu Lissu, Francis Stolla na Godwin Mwaipongo.

Mgombea mwingine wa nafasi hiyo,  Lawrence Masha, alitangaza kujitoa na kumuunga mkono, Lissu dakika za mwisho jana jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *