Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amedai kuwa hajashindwa kumlea mtoto wake Paula kama watu wanavyodai.

 

Kauli hiyo ya Kajala imekuja kufuatia watu kumlaumu muigizaji huyo ameshindwa kumlea mtoto wake kutokana na mtoto huyo kukosa maadili.

 

Kajala amsema kuwa anatamani awaoneshe watu hao malezi anayompatia binti yake huyo.

Muigizaji huyo amedai kuwa hawezi kushindwa kumlea mtoto wake na kwamba malezi anayompatia binti yake ni tofauti na yale watu wanayoyazungumzia katika mitandao ya kijamii.

Kajala ameongeza kwamba katika jambo linalomuumiza ni watu kutumia jina la binti yake hyo na kujifanya ni  yeye na wakati mwingine kuweka vitu vibaya ambavyo vinamfanya mtoto wake achukuliwe tofauti katika jamii.

 

Pia Kajala ameitaka serikali kushughulikia matatizo yanayotolewa na watumiaji wa mitandao  kwa umakini wa hali ya juu  ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu ya kutosha.

 

Paula ambaye ni mtoto wa muigizaji huyo pamoja na Producer P- Funky Majani aliwahi kukutwa na mkasa wa kufananishwa na binti aliyerekodiwa akiwa mtupu na kusambazwa mitandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *