Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane amembwatukia kocha wa sasa wa miamba hiyo Jose Mourinho na kudai ‘anaongea upuuzi’.
Keane amemshambulia kocha huyo kwa kauli yake ya kulalamikia ratiba ngumu kwa kikosi chake hali iliyopelekea kutolewa kwenye kombe la FA na vinara wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea.
Mourinho alikaririwa akisema ‘uchovu una gharama yake’ baada ya kumuona kiungo wake na mchezaji ghali zaidi duniani, Paul Pogba akitoka nje ya uwanja kwa kuchechemea wakati wa mechi ya kombe la Uefa kati ya United na FC Rostov usiku wa jana.
Hata hivyo Keane aliishambulia kauli hiyo kwa kusema: ‘Kwanini tusikilize upuuzi huu?’
‘Yeye ni kocha wa moja ya klabu kubwa duniani na kwa uwezo na ukubwa wa kikosi walichonacho hata wachezaji wa akiba wangeweza kushinda mechi ile’.