Mstahiki Meya wa Ubungo (CHADEMA) Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki.

Meya huyo amesema kuwa atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora.

Jacob ameeleza kuwa kesi hiyo itasimamiwa na mawakili maarufu Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Peter Kibatala.

Meya huyo ameamua kupeleka jambo hilo mahakamani ili kutambua uhalali wa jina la mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kama ni lake halali au amefoji.

Kesi hiyo itafunguliwa wiki ijayo baada mawakili hao kumaliza mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaotarajiwa kufanyika kesho  M ambapo Tundu Lissu ni mmoja wa wagombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi huo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anashtumiwa kuwa na vyeti feki na kutumia jina ambalo siyo lake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *