Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amevunja Bodi ya WETCU pamoja na  Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) kwa sababu ya kushindwa  kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo jana kwenye kikao na Bodi hizo kilichofanyika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora.

Pia waziri mkuu amesema, Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Bw. Vita Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Bw. Wilfred Mushi.

Waziri mkuu ameagiza kukamatwa kwa viongozi wa WETCU ambao ni Mwenyekiti Bw. Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa Ndani na Mhasibu Mkuu.

Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu wakulima wameteseka na zao hilo kukosa tija kwa sababu ya usimamizi mbovu wa viongozi wa ushirika na Bodi ya Tumbaku Tanzania jambo ambalo Serikali haiwezi kulivumilia.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa chama hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo limechangia wakulima wa tumbaku kukosa tija.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *