Marufuku ya kuzuia wahamiaji yaliyotangazwa na Rais wa Marekani, Donald Trump imepigwa marufuku na mahakama moja katika jimbo la Hawaii.

Marufuku hayo yalizuiwa saa chache kabla ya kuanza kutekelezwa saa sita usiku wa Alhamisi nchini humo.

Jaji wa Mahakama hiyo, Derrick Watson amesema ushahidi uliotolewa na serikali katika kutetea marufuku hiyo ni wa kutiliwa shaka.

Serikali ya Marekani ilikuwa imejitetea mahakamani ikisema marufuku hayo yanalenga kuimarisha usalama wa taifa.

Rais Trump ameeleza uamuzi huo wa jaji kuwa ni wakushangaza na akasema mahakama imevuka mpaka.

Agizo lililokuwa limetolewa na Trump, ambalo lilifaa kuanza kutekelezwa usiku wa kuamkia leo, ungepiga marufuku kwa miezi mitatu raia kutoka nchi sita zenye Waislamu wengi kuzuru Marekani nchi hizo ni Iran, Libya, Syria, Somalia, Sudan na Yemen.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *