Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Daimond Platnumz amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa jitihada zake kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa salama dhidi ya dawa za kulevya.
Diamond ameyasema hayo leo katika mkutano kuhusu vita dhidi ya madawa ya kulevya uliofanyika katika Bwalo la Polisi Oster Bay jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na viongozi wengine wa serikali na taasisi mbalimbali walihudhuria.
“Kwanza kabisa Nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda kwa jitihada zake. Ukizingatia ni mwaka mmoja tu tokea awe mkuu wa mkoa lakini utendaji wake umezaa matunda mengi na changamoto ni nyingi zinazo mkabili lakini bado amekuwa imara.”,
Pia Diamond Platnumz amempongeza mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, TID ambaye alitangaza kuachana na matumizi ya dawa za kulevya baada ya kuhisishwa na matumizi ya dawa hizo.