Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu na mwenzake leo wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na kesi inayowakabili ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kiasi cha gramu 1.08.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka umeileza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umefika hatua za mwisho.

Mwendesha mashtaka Constantine Kakula amedai hivyo leo mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati wa kutajwa kesi hiyo.

Katika kesi hiyo Wema na mwenzake wanakabiliwa na makosa matatu yanayohusiana na matumizi ya madawa ya kulevya aiana ya bangi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi April 11 baada ya upelelezi kutokamailika kwenye kesi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *