Klabu ya Azam leo inaondoka nchini kuelekea Swaziland kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane ya nchini humo.

Azam walifanikiwa kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza iliyofanyika katika  Uwanja wa Azam Complex, huku goli likifungwa na Ramdhan Singano.

Mechi hiyo ya marudiano inatarajiwa kufanyika Jumapili ya wiki hii kuko Swaziland ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya pili.

Ofisa habari wa timu hiyo, Jaffar Idd amesema kuwa msafara huo utaongozana na viongozi wa timu pamoja na wa viongozi kutoka TFF.

 “Kwanza nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote waliokuja kutusapoti kwenye mchezo wetu wa kwanza ambao tulishinda 1-0, licha ya siku ile mvua kunyesha, lakini mashabiki walijitolea kutushangilia mpaka tukapata matokeo yale.

“Kwa sasa tunaenda kwao kucheza mchezo wa marudiano ambapo kesho Jumatano ndio tunatarajia kuondoka tukiwa na wachezaji 23, viongozi kadhaa wa timu pamoja na wale wa TFF, lakini pia tayari kuna baadhi ya viongozi wameshatangulia kuweka mazingira mazuri ya kufikia timu,”.

Azam inatakiwa kushinda au kupata sare ya aina yoyote kwenye mechi hiyo ili kufuzu hatua inayofuata kwenye kombe hilo la Shirikisho barani Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *