Mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam leo imesababisha mafuriko baadhi ya maeneo ya jiji hilo.

Mafuriko hayo yamelikumba Bonde la Mto Mkwajuni lililoko eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo kuanzia asubuhi .

Bonde hilo zamani lilikuwa na watu wakiishi ndani yake kabla ya  kuondolewa na serikali kwa madai ya kuwa eneo hilo ni hatarishi kwa maisha yao kutokana na kuja maji wakati wa mvua.

Maeneo mengine yaliyokumbwa na mafuriko hayo ni bonde la Jangwani ambapo maji yalifurika maeneo hayo na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.

Mvua hizo zilianza kunyesha wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo mtu mmoja alipoteza maisha kutokana na mvua hizo lakini mvua ya leo haikusabisha kifo cha mtu yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *