Ujerumani imeiomba Tanzania kuiunga mkono katika harakati zake za kutafuta nafasi katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa uchaguzi utakaofanyika mwaka 2018.
Ujumbe wa Ujerumani umewasilishwa Tanzania na mjumbe maalum wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kwa Rais Dkt John Magufuli na balozi Harro Adt,na kusema nchi yake inaomba nafasi hiyo huku ikiwa na agenda nne muhimu.
Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Dkt Agustine mahiga amesema wanatambau mchango wa Ujerumani kwa taifa na afrika kwa Afrika kwa ujumla.
Katika kutafuta nafasi hiyo katika Baraza la usalama la umoja wa mataifa nchi tatu zitakuwa zikiwania nafasi moja huku Isarel na Ujerumani zikipigiwa upatu zaidi.