Mwanachama mkongwe wa CCM, Sophia Simba amevuliwa uanachama wa chama hicho huku wanachama wengine ambao ni Emmanuel Nchimbi na Adam Kimbisa wakipewa onyo kali.
Chanzo cha Simba kuvuliwa uanachama na wenzake kupewa onyo, ni madai ya kukisaliti chama, hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2015.
Habari zaidi zinaeleza kuwa wengine waliofukuzwa uanachama ni Ramadhan Madabida ambaye ni mwenyekiti wa mkoa wa Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Mkoa wa Iringa, Mwenyekiti wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa Mkoa wa Shinyanga. Habari zaidi zitaendelea kukujia kupitia hapahapa.
Orodha ya wote walioadhibiwa ni kama ifuatavyo
Wenyeviti wa Mikoa waliopewa onyo kali.
- Jesca Msamba Tavangi – Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa
- Erasto Izengo Kwirasa -Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga
- Ramadhani Rashid Madabida – Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam
- Christopher Sanya –Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM
- Ally Hera Sumaye – Wilaya ya Babati -amefukuzwa uanachama
- Mathias Erasto Manga – Wilaya ya Arumeru -amefukuzwa uanachama
- Ally Mchumo – Kilwa -amepewa onyo kali.
- Ajili Karoro -Wilaya ya Tunduru -Ameaachisha uongozi
- Hassan Masala- Singida- Ameachishwa uongozi atakuwa kwenye uangalizi kwa miezi isiyopungua 30, hataruhusiwa kujishughulisha na kazi yoyote ya chama.
- Valerian Alemreta – MNEC- Kibaha Vijini, ameachishwa uongozi.
Wenyeviti wa Wilaya wa CCM
- Omary Awadhi- Mwenyeviti wa Wilaya ya Gairo -Amefukuzwa uanachama
- Ally S. Msuya- Mwenyeviti wa Wilaya ya Babati Mjini -Amefukuzwa uanachama
- Makoi S Laiza -Mwenyeviti wa Wilaya ya Longido.
- Abel Kiponza -Mwenyeviti wa Wilaya ya Iringa Mjini – ameachishwa uongozi
- Salum Kondo Madenge – Mwenyeviti wa Wilaya ya Kinondoni – amefukuzwa uanachama
- Assa Simba Harun –Mwenyeviti wa Wilaya ya Ilala – Ameachishwa uongozi uanachama
- Wilfred Ole Morel – Mwenyeviti wa Wilaya ya Arusha Mjini – Amefukuzwa uanachama
- Hamis J. Nguli- Mwenyeviti wa Wilaya ya Singida Mjini- Ameachishwa uongozi.
- Muhaji Bishako – Mwenyeviti wa Wilaya ya Muleba -Amepewa onyo kali
Viongozi wa Jumuia Waliopatikana na makosa
Josephine Genzabuke – Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Mkoa wa Kigoma – amepewa onyo kali.
Sophia Simba – Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa – amefukuzwa uanachama.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa
Emmanuel Nchimbi—Mjumbe Kamati Kuu – amepewa onyo kali, anatakiwa kuomba radhi wanachama, uongozi na Chama Cha Mapinduzi kwa makosa ya kiuadilifu aliyotenda aliyotenda, atatakiwa aombe radhi huko huko aliko Ubalozini nchini Brazil.
Adam Kimbisa – Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki – Amesamehewa makosa yake anaweza kuendelea na kazi zake.