Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange amewataka Watanzania kuendeleza umoja, mshikamano na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuilinda nchi.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa gwaride la kuwaaga majenerali wastaafu 11 lilolilofanyika Kambi ya Twalipo Mgulani jijini Dar es Salaam.
Pia Mwamunyange ametoa rai kwa Jeshi la Polisi kuendeleza uzalendo, nidhamu iliyopo sasa ili kuimarisha weledi na kulifanya jeshi hilo kubaki na sifa.
Jenerali huyo pia alisema pamoja na changamoto zilizokuwepo katika jeshi hilo wakati akiwa kiongozi ikiwamo ufinyu wa bajeti na hivyo kushindwa kukidhi mahitaji yote jeshi liliendelea kuwa na nidhamu umahiri,weledi na kuwa mafano kwa majeshi mengine duniani..
Alimuomba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa sasa Jenerali Venus Mabeyo kuendeleza yale mazuri yaliyopo na kujali maslahi ya maofisa na kuangalia kero zao ili kujenga msingi mzuri.
Wengine walioagwa katika gwaride hilo ni pamoja Brigedia Jenerali Sara Rwambali, Brigedia Jenerali Josia Makere, Brigedia Jenerali Methew Sukambi, Brigedia Jeneral Joseph Chengelela na Meja Jenerali Rugashian Laswai.