Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuacha woga na waamshe mori ya kupigania haki ikiwamo kuirejesha Arusha ya Mwaka 2010.

Lema ameyasema hayo jana wakati akiwahutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Ngarenaro mjini hapa

Katika mkutano wake huo wa kwanza tangu alipotoka mahabusu ya Gereza la Kisongo alikokaa kwa miezi minne kutokana na kukosa dhamana ya kesi ya uchochezi inayomkabili.

 Lema amesema umefika wakati wa kupigania haki pale inapovunjwa na viongozi akiwamo Rais John Magufuli.

Mbunge huyo amesema kuwa “Hatutaogopa kumkosoa Rais Magufuli pale atakapokuwa amevunja Katiba ya nchi, tutasema kweli na tutapigania haki hiyo,”.

Akielezea kuhusu kukaa kwake mahabusu miezi minne Lema aliyekuwa akishangiliwa kila alipozungumza alisema, wito wa uongozi na kuwatumia wananchi ndio uliomsukuma kukaa magereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *