Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rumishael Shoo A.K.A  Rummy anashikiliwa na Jeshi la Polisi makao mkauu (Central) kwa tuhuma za kujihusisha na madawa ya kulevya.

Hayo yamesemwa na kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu usalama wa jiji hilo.

Kamanda Sirro amesema kuwa mwanamuziki huyo anahojiwa kuhusu tuhuma hizo na pamoja na kupelekwa kwa mkemia mkuu wa Serikali na akipatikana na hatia atafikishwa mahakamani kutokana na tuhuma hizo.

Pia Sirro amesema kuwa Vanessa Mdee bado anashikiliwa na jeshi hilo kutokana na tuhuma hizo za kujihusisha na madawa ya kulevya ambapo alitajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kwa upande mwingine Kamanda Sirro amesema kuwa jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limewakamata wahalifu mbali mbali, Silaha na magari mawili aina ya Noah yaliyokuwa yanatumika kwenye uhalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *