Muziki wa sasa umekuwa biashara kubwa mno na wasanii wengi wanajaribu kutoka kwenye level ya kuimba na kutunga nyimbo tu na kuhamia kwenye kuwa mameneja.
Mmoja kati ya wasanii ambaye anaonekana kufanikiwa kwenye kuliteka soko la muziki wa Bongo na sasa anataka kuwaajiri wasanii wenzake ni Diamond Platnumz.
Unaujua mkakati wake?
Hebu tazama kwa makini hatua hizi kisha tafakari anakoelekea:
1: Ameanzisha label ya WASAFI kwaajili ya kuwasaini wasanii (kila aliye bora atakayeridhiwa na menejimenti ya WCB)
2: Studio….kisha staa huyo akaanzisha studio kwaajili ya wasanii kurekodi ngoma zao kwa malipo au kwa makubaliano mengine (ikiwemo kusainishwa na lebo hiyo)
3: Kusaini mikataba ya kibiashara ya kimataifa (Njia ya kuwaonyesha wasanii kuwa kwa kufanya kazi na yeye, wana uhakika wa mafanikio siku za mbele)
4: www.wasafi.com na sasa Diamond ameanzisha tovuti maalum kwaajili ya kutangaza kazi za wasanii na wakati huo huo kuuza kazi za wasanii kupitia mtandaoni.
Biashara hii ilikuwa ikifanywa na makampuni mbalimbali ambayo pia Diamond alikuwa mteja wao.
Je, hii sio njia ya kuwakusanya mastaa wa Bongo na kuwapa opportunity ya kukua kimataifa? Lakini pia, Diamond Platnumz anawekeza kwenye namna ya kuwafanya wasanii wa Tanzania wafanye kazi kwa niaba yake kwenye miaka ijayo.
Is Diamond Platnumz new Jay Z in Tanzania?