Idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya Mkoa wa Mbeya imeongezeka kutoka asilimia Idadi 20 hadi kufikia asilimia 25 kwa miaka  tofauti.

Takwimu hizo zimetolewa jana na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya Akili, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dk. Paul Lawala, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla.

Dk. Lawala alisema kama hali hiyo isipodhibitiwa inaweza kuwa mbaya zaidi.

Amesema kuwa “Hali inazidi kuwa mbaya zaidi na zinahitajika nguvu za ziada ili kukabiliana na hali hiyo vinginevyo waathirika watazidi kuongezeka,” alisema Dk. Lawala.

Naye Makalla alikemea matumizi ya dawa hizo na kusema yeyote atakayekamatwa akijihusisha na biashara ya dawa hizo, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Vyombo vya ulinzi na usalama lazima muwe macho kudhibiti matumizi ya dawa hizo na yeyote mtakayemkamata mfikisheni katika vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Makalla.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, alisema idadi kubwa ya waathirika wa dawa hizo ni vijana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *