Muimbaji wa muziki wa asili, Saida Karoli amesema kuwa mikataba aliyosainishwa na aliyekuwa Meneja wake ilikuwa siyo sahihi kwasababu hakuwa anajua kusoma na kuandika.

Saida Karoli amesema kuwa album tano alizofanya huko nyuma hana haki nazo na meneja wake wa zamani ndio mwenye haki nazo.

Pia mwanamuziki huyo amesema kuwa kuhusu Diamondo kurudia nyimbo yake ana hesabu kama alitoa bure kwani hata fedha aliyopewa ni kidogo na haifai kuongelea.

Saida ameongeza kwa kusema kuwa “Meneja wa zamani aliniuliza nyimbo yako inatakiwa kutumika lakini nipe idhini yako japo ni nyimbo zangu zote lakini sikuwa na haki licha ya kuwa sauti yangu imesikika kule.

“Walizushaga nimekufa na nilihisigi nimekufa kweli kutokana na hali ya maisha na nilikuwa nimekata tamaa nikajua nimekufa kweli” Alisema Saida Karoli

Kwa sasa Saida yupo Dar na amekuja rasmi kwa ajili ya kufanya muziki upya kama zamani na yupo tayari kufanya kolabo na wasanii kama Ben pol, Bell 9, Diamond na Darassa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *