Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewataka wataalamu wa Ofisi ya Madini kufanya utafiti wa kutosha wakati wa utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini ya dhahabu mkoani humo.

Makalla amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza kero, migogoro na malalamiko baina ya wachimbaji wadogo, wa kati na wale wakubwa.

Mkuu wa mkuoa huyo amesema kuwa wataalamu wamekuwa wakifanya kazi kupitia mafaili ofisini na kujikuta wakitoa maamuzi yasiyo sahihi badala ya kutoka nje kwenda kujiridhisha katika maeneo husika, hivyo kuchangia kuibua kero na migogoro kwa wachimbaji wadogo na wawekezaji.

Amesema ofisi hiyo inapaswa kujiridhisha kwa kufika kwenye maeneo ya ardhi, hasa yale yanayoombwa na wachimbaji wadogo kwa ajili ya kuyakagua na kisha kutoa leseni, lengo likiwa ni kupunguza malalamiko.

Pia Makala aliahidi ofisi yake kuyafanyia kazi malalamiko yote yaliyotolewa na wananchi, wakiwamo wachimbaji wadogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *