Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.

Mwanasheria wake, Aman Tenga ametihibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Tenga pia ametihibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa.

Pia aliongeza kuwa Polisi walikwenda Nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.

Vanessa ni miongoni mwa wasanii waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaojihusisha na biashara ya dawa za kuleva.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *