Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ameiagiza bodi mpya ya VETA kuwawajibisha viongozi wa mamlaka hiyo kwa kutotekeleza miradi yao.

Profesa Ndalichako ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa bodi mpya ya Veta.

Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa fedha za miradi hiyo lakini hakuna hata mradi mmoja uliotekelezwa.

Profesa Ndarichako amesema kuwa “Yaani ile dhana ya hapa kazi tu Veta haipo hata kidogo, Veta ni ubabaishaji hivi kuna faida gani kumweka mkurugenzi.

Pia amesema katika taasisi yako malengo yako ya mwaka mzima hakuna hata lililotekelezwa na fedha unazo, yaani turudishe fedha kwasababu mtu ameshindwa kutumia? Mkurugenzi wa namna hiyo Mwenyekiti unamhitaji?alihoji Ndalichako.

Ameongeza kwa kusema “Bodi mnahitaji kuwa na wakurugenzi wa namna hiyo, mtu anakaa mwaka mzima hajatimiza hata kitu kimoja na fedha serikali imempatia, hatuhitaji kuwa na wakurugenzi wa namna hiyo katika taasisi zetu kwahiyo naomba bodi nyie kisheria ndiyo wenye mamlaka ya kuona nani anafaa kuwa mkurugenzi naomba hata wakurugenzi wote ikiwezekana hata mbadilishe mfumo muweke kwa mkataba au ikiwezekana akae kwenye cheo kutokana na matokeo ya kazi.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *