Mama mlezi wa aliyekuwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, Bi Nuru Kikwete amefariki dunia katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwan Kikwete ambaye ni mjukuu wa marehemu, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho asubuhi ya leo.
Kupitia ukuras wake Instagram Ridhwani ameandika “Ndugu na marafiki nasikitika kuwatangazia msiba/kifo cha Bibi yetu Bi. Nuru Khalfan Kikwete kilichotokea asubuhi hii katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Taratibu za mazishi tutajulishana” .