Mahakama nchini Tanzania imemhukumu kifungo cha miaka 12 gerezani mtuhumiwa sugu wa mauaji ya Tembo na usafirishaji wa pembe za ndovu, Boniface Mariango maarufu kama ‘Shetani’.

Kwa mujibu wa taasisi ya kulinda wanyama pori, Boniface Matthew Mariango anadaiwa kuhusika na mauaji ya Tembo zaidi ya elfu moja na alikamatwa jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka jana baada ya kusakwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Makosa ya uhalifu wa Maliango yanadaiwa kuwekwa wazi kupitia makala ya televisheni iliyoandaliwa na kampuni ya Netflix iitwayo The Ivory Game, ambayo imechezwa na muigizaji mahiri wa Hollywood Leonardo DiCaprio.

Taasisi ya kuzuia mauaji ya wanyamapori wakiwemo Tembo ya ‘The Elephant Action League’ imedai kuwa imekuwa ikifuatilia kwa karibu mtandao wa mauaji ya Tembo na utoroshwaji wa pembe za Ndovu kwenye nchi za Tanzania, Burundi, Zambia, Mozambique and southern Kenya.

Maliango amehukumiwa kifungo hicho sambamba na ndugu yake Lucas Mathayo Mariango na Abdallah Ally Chaoga.

Watu hao walikamatwa mwaka 2015 wakijaribu kutorosha shehena ya pembe za ndovu iliyokuwa na thamani ya $850,000 (TZS 1.9bn).

Mariango anatuhumiwa kuwa msambazaji mkuu wa pembe za Ndovu kwa raia wa China, Yang Fenglan maarufu kama Malkia wa Pembe Ndovu, ambaye bado anaendelea kufuatilia mashtaka yake kwenye mahakama ya Kisutu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *