Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema kwamba tukio hilo limetokea jana katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa jiji mmoja (01) walijeruhiwa.

Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya barabara.

Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.

Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *