Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ametoa siku saba kwa Wizara ya Nishati na Madini kumpatia mfanyabiashara, Aliko Dangote eneo la kuchimba makaa ya mawe.
Rais Magufuli ametoa maagizo hayo mkoani Mtwara kabla ya kuzindua magari 580 ya Dangote yatakayokuwa yakibeba saruji kutoka kiwanda cha mfanyabiasharahuyo.
Magufuli ameagiza kuwa makaa ya mawe yakiisha kwenye eneo atakapopewa Dangote, apewe eneo lingine ili kuhimarisha sekta ya viwanda nchini.
Aidha Magufuli amemruhusu Dangote auze makaa hayo kwa watu wengine ili serikali ipate fedha kutokana na makaaa ya mawe hayo
Pia ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kukusanya mapato ya uchimbaji wa makaa hayo kwa Dangote mwenyewe.
Rais Magufuli amemhakikishia Dangote kuwa, ndani ya siku hizo atakuwa amepata kibali cha kuchimba makaa ya mawe kwa ajili ya kiwanda cha saruji kilichopo Mtwara.