Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.

Mkuu wa mkoa amesema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.

Amesema katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.

Amesema kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi imara.

Pia amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *