Muigizaji wa Bongo Movie,  Jacqueline Wolper amesema kuwa  amekerwa na mwanamuziki Harmorapa baada ya kumuimba kwenye nyimbo kuwa ametoka nae kimapenzi.

 Wolper amesema mwanamuziki huyo ambaye amemuimba kwenye wimbo wake wa Kiboko ya Mabishoo kuwa ameshatoka naye kimapenzi jambo ambalo siyo kweli.

Muigizaji huyo amesema kuwa  rapa huyo amemkosea heshima  na hata alivyousikia wimbo huo umemshangaza kwa sababu hata Harmorapa mwenyewe anamuona kwenye mitandao ya kijamii na magazetini tu hajawahi kuonana nae.

harmorapa

Wolper ameongeza kwa kusema kuwa “Jamani huku ni kukoseana heshima maana huyo Harmorapa hata simfahamu huwa namuona kwenye mitandao na magazetini tu, sasa alivyoimba ametoka na mimi kimapenzi naona kama ni kituko kikubwa sana.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *