Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa anajivunia uamuzi wake wa kutojihusisha na siasa maana amepata amani ya moyo kuliko wasanii wenzake ambao kwa sasa  wapo kwenye malumbano ya kisiasa.

Lulu amesema hayo baada ya wasanii wenzake kulumbana kuhusu siasa kwa kutupiana vijembe kupitia mitandao ya kijamii.

Lulu amesema kuwa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu Mwaka 2015, watu wengi walikuwa walikuwa hawamuelewi lakini ukweli ni kwamba aliliona hili ambalo linatokea kwa sasa ambapo wasanii wanaumbuana, wanasemana na kuwagawa mashabiki.

“Unajua watu wengi walikuwa hawanielewi kwa nini sipendi siasa na ninajua wazi wengi waliniona labda mimi naringa sitaki kujumuika na wezangu lakini siyo hivyo nilijua nini kinaweza kutokea mbeleni kama ilivyo sasa,” alisema Lulu kufafanua anazungumzia malumbano yapi hasa.

Muigizaji Wema Sepetu alitangaza kujitoa CCM na kujiunga na Chadema ambapo alitupa dongo  kwa CCM kwa kusema anawadai hela za kampeni hali ambayo iliwaibua wasanii wenzake, kumpinga vikali kwa maelezo kuwa walilipwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *