Baada ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuachiwa kwa dhamana leo na mahakama kuu kanda ya Arusha, Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu ametumia akaunti yake ya Instagram kumpongeza mbunge huyo.
Wema Sepetu kupitia akaunti yake ya Instagram ameweka picha ya mbunge huyo ikiambatana na maelezo ya kumpongeza baada ya kuachiwa kwa dhamana na mahakama ya kuu kanda ya Arusha.
Mbunge huyo anakabiliwa na shitaka la uchochezi ambapo alikamatwa mwezi Septemba mwaka jana akiwa Bungeni Dodoma na kupelekwa Arusha kwa ajili ya kufunguliwa shitaka la uchochezi.
Wema Sepetu ambaye hivi karibuni amehama Chama Cha Mapinduzi na kuhamia Chadema ameandika maneno yafuatayo ” Mungu ni mkubwa…..Ni furaha kusikia Mh Godbless Lema amepewa dhamana…… Najua ulipitia wakati mgumu sana..Ulikuwa mbali sana na familia yako, watoto wake.
Hayo ni baadhi ya maneno alioandika Wema Sepetu kwenye ukurasa wake Instagram akiambatanisha na picha ya Lema.